Tunafanya Nini

Msaada kwa Viwanda vya Mbao vya Kadri, Kati na Vidogo

Walengwa wengine wakubwa wa Programu ya Panda Miti Kibiashara mbali, na wakulima wa miti, ni viwanda vinavyojihusisha na shughuli za kulanda mbao. Viwanda hivi ni vile vya kadri, kati na vidogo. Msaada kwa viwanda hivi hutolewa katika namna mbili; mafunzo kwa makampuni husika na huduma ya uanzishwaji na uboreshaji wa biashara kwa makampuni machache yaliyoteuliwa kupata huduma hii katika mwaka husika.

Uwekaji wa mashine ya mafunzo ya uchakataji/upasuaji magogo/mbao utafanyika katika mikoa wa Nyanda za Juu Kusini kusaidia katika shughuli ya mafunzo. Itawekwa mashine za kisasa na vifaa vitakavyokidhi mahitaji ya sehemu hiyo na vinavyoweza kupatikana kwa urahisi.