Tunafanya Nini

Walengwa

Walengwa wa Programu ya Panda Miti Kibiashara ni wale wanaonufaika na uboreshwaji wa utendaji katika mfumo mzima wa kilimo cha miti. Programu imeratibiwa  kwa ajili ya kuboresha hali za maisha za  wakulima wa miti katika mikoa ya:

  • Iringa (wilaya za Mufindi na Kilolo);
  • Njombe  (wilaya za  Njombe na Njombe TC);
  • Morogoro (wilaya za Ulanga na Kilombero);
  • Ruvuma (wilaya ya Songea).

Vilevile Programu inalenga katika kuboresha  maisha ya watu na kaya mbalimbali, viwanda vidogo na vya kati na sekta ya misitu kwa ujumla.

Vikundi vya wakulima wa miti vinatumia mbinu shirikishi na kuhakikisha kuwa wakulima wanawake wanapata fursa ya kuwa wanachama. Vilevile shughuli za kiabishara ambazo zinaimarishwa kwa msaada wa Programu hii zitatoa fursa za ajira kwa watu kwenye mashamba au viwanda vya kadri, vidogo na vya kati. Watu walio katika makundi maalum watapewa upendeleo katika utoaji wa ajira.

Pamoja na hayo, Programu kwa kushirikiana na Shirika la 4H Tanzania, imeanza kutekeleza shughuli za kilimo cha miti katika shule kadhaa. Kwa ushirikiano huo, mamia ya wanafunzi watafikiwa  na klabu nyingi za 4H zitaanzishwa.