Tunafanya Nini

Tunafanya Nini

Programu imelenga kuinua kipato katika maeneo husika ambayo ni wilaya tisa za Nyanda za Juu Kusini na bonde la Kilombero. Programu inalenga katika kupunguza umaskini na kuleta usawa katika jamii hizo kwa  kuboresha kilimo cha miti  kilicho endelevu na kuongeza thamani katika hatua zote za  uzalishaji wa mazao ya misitu tangu upandaji wa mbegu bora hadi uuzaji wa mazao bora ya misitu sokoni.

Katika kufanikisha hili, Programu

  • itawezesha jamii husika katika kupanga Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ulio shirikishi na endelevu;
  • Kuwawezesha wakulima wa miti kujikusanya na kuunda Vikundi vya Wakulima wa Miti (Tree Growers’ Associations -TGAs);
  • kuwajengea uwezo wakulima wa miti;
  • kusaidia katika uanzishwaji wa mashamba na kiuimarisha usimamizi wake;
  • kuimarisha huduma za ugani na biashara na
  • kubooresha uzalishaji katika viwanda hasa viwanda vidogo na vya kati.
  • Programu itabuni mbinu mpya mbalimbali ambazo zitafanyiwa tathimini na zile zitakazodhibitika kua bora Zaidi zitapendekezwa kutumika kwenye sekta ya misitu.

Shughuli kuu ya Programu ni kuwasaidia wamiliki wadogo wadogo wa mashamba ya miti na kuvisaidia viwanda vidogo vidogo vya mbao kupiga hatua kibiashara. Msaada hutolewa katika mfumo wa huduma za ugani, mafunzo na uwezeshwaji wa shughuli za kibiashara.

Progrmu pia itasaidia katika kuleta maendeleo ya sekta nzima ya misitu kwa kuratibu majadiliano baina ya wadau na kutoa mapendekezo kwa ajili ya sera, sheria na maendeleo ya biashara ya mazao ya misitu. Vilevile, Programu itawahamasisha  vijana  waishio katika maeneo ya kilimo cha miti  na  hifadhi za asili kushirikiana na  shirika la kuhimiza maendeleo mashuleni la 4H katika kushiriki katika shughuli za misitu.