Muundo wa Shirika la PFP

Vyombo vya usimamizi wa Programu na majukumu yake ni kama inavyoonekana katika mchoro hapo chini.

SUPERVISORY BODY- BODI YA USIMAMIZI

 kufanya maamuzi katika ngazi ya kitaifa.

STEERING COMMITTEE - KAMATI YA UENDESHAJI

  • Usimamizi wa shughuli za uendeshaji na kufanya maamuzi

PROGRAMME MANAGEMENT UNIT -  KITENGO CHA USIMAMIZI WA  PROGRAMU

  • Usimamizi wa  wa Programu  unaofanywa na Timu ya Usimamizi
  • Wafanyakazi wa timu ya ufundi
  • Kusaidia  katika shughuli za utawala

CONSULTANTS’ HOME OFFICE - OFISI KUU YA WATAALAMU WAELEKEZI

  • Kuratibu na kutoa msaada wa kitaalam.

 TASK TEAM - TIMU YA UTENDAJI

  • Utekelezaji wa majukumu  husika

PARTICIPATING STAKE HOLDERS - WADAU WASHIRIKI

OUTSOURCED SERVICE PROVIDER - WATOA HUDUMA KUTOKA NJE YA PROGRAMU

Dira

Dira ya Programu kwa sekta ya upandaji miti kibiashara Tanzania, ni kuwezesha uzalishaji wa kipato endelevu kwa jamii nzima katika sekta ya misitu na sekta nyingine amabatanishi huku ustawi endelevu wa jamii na mazingira ukizingatiwa katika uwekezaji huo.

Hii itaifanyaTanzania kuwa mzalishaji mkuu wa mbao kwa masoko la ndani na nje, na wawekezaji katika sekta ya upandaji miti na viwanda vya misitu wataziona Nyanda za Juu Kusini  kuwa ni moja ya maeneo muhimu na yenye tija  kwa  uwekezaji .

Dhamira

Lengo kuu la Programu ni upandaji miti endelevu kwa shabaha ya kuondoa umaskini na kukuza uchumi nchini.

Dhamira kuu ya Programu hii, ni kuanzisha na kuimarisha upandaji miti kibiashara ulio endelevu na jumuishi ili kuchangia katika kuinua kipato cha watanzania na kupunguza umasikini.

Katika harakati za kuwezesha wakulima wa miti wa Nyanda za Juu Kusini kuongeza kipato na ajira, haki za makundi maaluum zitalindwa na kuwawezesha kushiriki tangu hatua za awali za upandaji  miti hadi uuzaji wa mazao sokoni.

Lengo la awamu ya kwanza ya Programu hii (2014-2017), ni kuwezesha upandaji wa miti ulio endelevu, shirikishi na wenye faida kiuchumi na kuhakikisha kwamba shughuli ambatanishi zinatoa ajira  na kuongeza kipato kwa wamililiki  binafsi wa mashamba  ya miti, vikundi vya uzalishaji vidogo na vya kati na kaya za wasiojiweza zilizo katika eneo la Programu.